Chelsea yaishinda Peterborough United 4-1


Nahodha wa Chelsea John Terry alitimuliwa uwanjani dakika ya 66, baada ya kupewa kadi nyekundu, ambayo ndiyo yake ya kwanza tangu mwezi Oktoba wakati ambapo Chelsea wamewanyuka Peterborough mabao 4-1. Chelsea waliitawala mechi hiyo licha ya kukabiliwa na mashambulizi kadha kutoka kwa Peterborough. Terry alipewa kadi nyekundi baada ya kumchezea vibaya mshambulizi Angol. Kutimuliwa kwa Terry ni pigo kwa Chelsea ambao wameonyesha mechi safi baada ya kushindwa na Tottenham, ambacho ni kipigo chao cha kwanza kati ya mechi 11 walizocheza.

Post a Comment

Previous Post Next Post