Msanii wa muziki Bongo, Chid Benz amefunguka ukweli wa taarifa zilizodai kuwa ameamua kuokoka.
Taarifa hizo zimeibuka mara baada ya kuoneka katika moja ya makanisa, pia akiwa na muimbaji wa nyimbo za Injili, Bony Mwaitege.
Taarifa hizo zimeibuka mara baada ya kuoneka katika moja ya makanisa, pia akiwa na muimbaji wa nyimbo za Injili, Bony Mwaitege.
Rapper huyo akizungumza na EATV amesema alialikwa kanisani hapo kama mgeni rasmi wa shughuli iliyokuwa ikiendelea na hakuna zaidi ya hapo.
“Nilialikwa pale kama mgeni rasmi, kulikuwa kuna wabunge, wajumbe wa serikali, lakini mimi nilialikwa nisingeweza kukataa, tena nikaona ni bahati ni siku yangu ya kuzaliwa, nikaona kwa nini nisende nikasikiliza nikaungana nao, mimi ni Rashid Abdala Makwilo, sijabadilisha,” amesema Chidi Benz.
Tangu July, 2017 Chidi Benz alipotoa ngoma inayokwenda kwa jina Muda ambayo alimshirikisha Q Chillah hajatoa ngoma yoyote zaidi ya kugonga vichwa vya habari kwa matukio mbali mbali.
Tags:
Burudani