MBUNGE wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amesema kutokana tukio la kuuawa kwa mdogo wake Suguta Chacha kwa kuchomwa kisu na askari polisi haturudi nyuma kupigania haki za watu ili haki na usawa kushamiri katika nchi.
Heche amesema hayo leo Ijumaa, Mei 4, 2018 ikiwa ni siku moja baada ya mazishi mdogo wake huyo na kusema mdogo wake ameuawa kinyama, na kifo hicho kinazidi kumpa nguvu na sababu ya kupigania haki.
“Nakuombea, upumzike kwa amani Suguta, kifo chako cha kinyama kinanipa sababu zaidi ya kuendelea kupigania. Utawala wa sheria haki na usawa katika taifa letu. Sitarudi nyuma nitapambana mstari wa mbele wakati wote kwa heshima yako na kwa heshima ya Watanzania wote wanaopenda kuona nchi yetu inaongozwa vizuri,” alisema Heche.
Aidha, Heche amewashukuru waombolezaji waliojitokeza kumzika mdogo wake huyo kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa wamewapa faraja sana.
“Asanteni Watanzania wote na Wanatarime kwa jinsi ambavyo mmekua faraja kwa familia yetu katika kipindi hiki kigumu, endeleeni kupiga kelele kukemea uovu huu unaozalisha chuki katika Taifa letu. Pumzika kwa Amani “Simba””.
Tags:
Habari