Mwanamuziki wa Bongo fleva Barakah The Prince amekumbwa na skendo nzito ya kumpachika mimba mwanamke mwingine ambaye ni mchepuko wake na sasa anadaiwa kuikataa mimba hiyo.
Miezi michache iliyopita kuna tetesi zilisambaa kuwa Barakah alionekana mkoani Mwanza na mwanamke mwingine ambaye ilidaiwa ni mchepuko wake wakila bata Kwenye hoteli ya kifahari.
Barakah alikana tetesi hizo na kudai kuwa ana mpenzi mmoja tu ambaye ni Naj na hana mwanamke mwingine na wanaosambaza taarifa hizo wanataka kumuharibia penzi lake na Naj.
Shilawadu wanaripoti kuwa msichana huyo mwenye kibendi cha Barakah anaitwa Naomi na ni mkazi wa Arusha na inasemekana hivi sasa Barakah anakataa mimba hiyo na tayari msichana huyo amesha mtafuta Naj kumuuliza.
Kwenye mahojiano na XXL ya Clouds Fm, Mchepuko huyo wa Barakah The Prince alifunguka haya kuhusiana na taarifa hizo:
"Nina mimba ya Barakah lakini hataki Habari za hiyo mimba na mimi nimeshamwambia mwanamke wake Najma. Mimi ninachotaka huyo barakah afikirie na atoe jibu moja kuhusi hii mimba maana mimi siwezi kutoa hii mimba".