Kijana Frank Joseph mwenye umri wa miaka 23 ambaye anaishi Dar es Salaam, Mbezi Mwisho amefunguka na kusema kuwa ni kweli aliiba mzigo huo japo kwake ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kumuibia mama huyo.
Kijana Frank amesema kuwa baada ya kuiba mzigo Mlandizi mkoani Pwani baadae ulikataa kutoka kichwani mpaka pale alipopigiwa simu muhusika ndipo alikuja kutokea Dar es Salaam ambako anafanya kazi na kufika kituo cha polisi Mlandizi kisha alimshika zipu ndipo alipoweza kushusha mzigo huo wa mahindi kichwani.
"Ni kweli nimeiba na sasa nashikiriwa na serikali kwa wizi na mzigo ulikuwa hautaki kushuka mpaka mama huyo alipofika na kunishika zipu kwa msaada wake ndiyo mzigo huo uliweza kushuka, kwa mimi ni mara ya kwanza kumuibia huyo mama labda sijui kwa watu wengine, mimi nilikuwa napita tu nilipouona mzigo huu nikachukua na kuondoka nao"
Aidha kijana huyo Frank Joseph kufuatia tukio ambalo limekuta leo amewaomba vijana wengine ambao wanajihusisha na wizi kuacha kufanya hivyo akisema ni si jambo zuri pia Kamanda Shana amewataka vijana wafanye kazi badala ya kutaka kufanya vitendo vya uharifu ambavyo vitawagharimu maisha yao.
Tags:
Habari