Ni Bora Ule Sumu Kuliko Kula Hela ya Serikali ya Awamu ya Tano-Rais Magufuli.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kula hela za serikali ni sawa na kula sumu na nafuu ule sumu kuliko kula hela ya serikali ya Awamu ya Tano.



Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mkoa Morogoro katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara mkoani Morogoro amesema kuwa haiwezekani yeye ahaingikie kukusanya hela kutoka kwa wananchi masikini alafu wanakula.

“Kuna baadhi ya miradi makandarasi wamekula pesa, nataka kuwahakikishia hao wakandarasi wamekula sumu, hela za serikali haziliwi, ni nafuu ukale sumu kuliko kula hela za serikali ya awamu ya tano.Haiwezekani mimi nihangaike kukusanya hela kutoka kwa wananchi masikini, halafu unapewa kandarasi we uende kuila, nataka kuwaeleza wakandarasi mmekula wa chuya,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli amempigia simu live, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo mbele ya wananchi wa kijiji cha Kidodi Morogoro kutaka kumchukulia hatua mkandarasi aliyepewa kutekeleza mradi wa maji wa kijiji hicho, ambaye alishapewa pesa za mradi milioni 800 na maji hayajafika kwa wananchi .

Post a Comment

Previous Post Next Post