Usiku wa May 1 2018 mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya FC Bayern ulichezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid nchini Hispania, Bayern wakiingia na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani kwa magoli 2-1.
FC Bayern wakiwa ugenini walianza na kasi na dakika ya 3 ya mchezo wakafanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Joshua Kimmich, mabo yalibadilika kuanzia dakika ya 11 baada Karim Benzema kufunga goli la kusawazisha na dakika ya 46 akafunga goli la uongozi lililodumu hadi dakika ya 63 James Rodriguez alipoisawazishia FC Bayern.
Dakika 90 ikamalizika kwa sare ya kufungana magoli 2-2 lakini Real Madrid wamefanikiwa kuingia fainali ya UEFA Champions League itakayochezwa mjini Kyivkatika nchi ya Ukraine kwa ushindi wa jumla ya aggregate ya magoli 4-3, hivyo Real Madrid wanasubiri mshindi wa mchezo wa kesho kati ya AS Roma dhidi ya Liverpoolkufahamu watacheza na yupi fainali.
Tags:
Michezo