Staili ya Ushangiliaji ya Haji Manara ya Ushangiliaji Yamtokea Puani Apewa Onyo Kali na Kamati ya Ulinzi.


Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wake Yanga mwishoni mwa wiki.

Furaha hiyo ilimfanya msemaji wao kuingia uwanjani kumalizia shangwe na mashabiki wao.

Lakini Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei Mosi, 2018 chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.


Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepewa Onyo Kali kwa kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.

Kitendo chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Post a Comment

Previous Post Next Post