Waziri Mahiga Aomba Radhi kwa Rais Magufuli Kisa Hiki Hapa.


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustino Maiga ameomba radhi kwa Rais Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa kukosa kura 25 za udhamini kipindi cha kampeni za uchaguzi 2015.

Balozi Maiga ameomba radhi hiyo leo kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa inafanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa.

“Nakumbuka Mhe. Rais ulipata shida kidogo kupata wadhamini hapa Iringa Mjini ikabidi utoke nje ya mji ndiyo ukapata ila wadhamini 25 kwa hapa mjini kura hazikupatikani tunakuomba radhi sana Mhe. Rais kwa kukosa busara hiyo. Lakini ulipokuwa hapa ulitoa ahadi kwa wana Iringa na umezitimiza ahadi ya kwanza ulisema Iringa itakuwa Makao Makuu ya Utalii ya mikoa ya kusini hilo tumeshalifanya, Mkuu wa mkoa aliitisha vikao na watu wa mikoa mingine lakini hasa wewe umeshafanya maamuzi kuwa Uwanja wa ndege wa Iringa wa Nduli utarekebishwa na kuweza kuchukua ndege kubwa zaidi kama zile za Bombidier,” alisema Dkt. Mahiga.

Post a Comment

Previous Post Next Post