Msanii wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, akizungumza jambo kwa niaba ya wasanii wenzake mara baada ya kutambulishwa rasmi kuwa mabalozi wa StarTimes.
Mkurugenzi wa StarMedia Tanzania, Wang Xiaobo, mwenye suti akiwakabidhi madishi ya televisheni mabalozi hao.
…Akijiandaa kupiga mpira ulio mbele yake kuashiria rasmi shughuli ya uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa StarTimes, David , akielezea namna watakavyofanikisha zoezi la urushaji matangazo yote ya kombe hilo.
Meneja Maudhui wa StarTimes, Zamaradi Nzowa (wa kwanza kushoto) akiwatambulisha rasmi wasanii hao kuwa mabalozi wao.
Wasanii wakiwa kwenye picha na baadhi ya viongozi wa StarMedia.
Baadhi ya wanahabari waliohudhuria shughuli ya uzinduzi huo wakichukua matukio mbalimbali.
KAMPUNI ya StarMedia, imetoa shavu la ubalozi kwa staa wa filamu Bongo. Wema Sepetu na wenzake, ambapo atakuwa na kazi ya kuhamasisha baadhi ya watu kuhakikisha wanafuatilia matangazo ya Kombe la Dunia, litakapoanza Juni 14 mwaka huu nchini Urusi.
Wema ataungana na baadhi ya wasanii kama Madee, Kitale, Mkaliwao, Bitoke, Manifongo na Monalisa, ambao watatumia sanaa yao kufikisha ujumbe kwa wapenda soka wote ndani na nje ya nchi.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa, leo alisema uzinduzi huo unaashiria rasmi harakati za mwanzo za kuonyesha kombe hilo litakaloonyeshwa kupitia Channel zake za michezo za World Football na Sports Premium kwa muda wote wa mashindano hayo huku likitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.
Meneja Maudhui wa StarTimes, Zamaradi Nzowa, ametumia muda kuwatangaza mabalozi wao ambao watakuwa na jukumu la kufanya kazi hiyo ya kutoa hamasa kwa muda wote wa mashindano hayo.
Tags:
Burudani