Rais wa TFF Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Mchezaji wa Zamani wa Taifa Stars

Rais wa TFF Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Mchezaji wa Zamani wa Taifa Stars

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Ndugu Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Rajabu Digongwa aliyefariki huko mkoani Tanga.

Rais wa TFF Ndugu Karia amepokea kwa huzuni na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha mchezaji huyo wa zamani aliyefariki baada ya kuugua.

Kwa niaba ya TFF Rais wa TFF Ndugu Karia ametoa pole kwa familia ya mchezaji huyo ,wanafamilia wa Mpira wa Miguu,ndugu ,jamaa na marafiki.

“Marehemu Digongwa namfahamu vizuri toka enzi akicheza na kifo chake kimenishtua na kunihuzunisha kwa niaba ya TFF natoa pole kwa wafiwa" alisema Karia.

Enzi za uhai wake marehemu Digongwa alicheza timu za Wananchi FC, African Sports, pia alipata kuitwa kwenye timu ya mkoa wa Tanga na pia timu ya Taifa ya Tanzania.

 Mazishi ya marehemu Digongwa yamefanyika leo saa 4 asubuhi mkoani Tanga

Wakati huohuo Rais Karia pia ametuma salamu za rambirambi kwa mchezaji wa zamani Khalid Bitebo aliyefiwa na mkewe.

Ametoa pole kwa Bitebo na familia kiujumla akiwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post