BREAKING NEWS: Mahakama yaamuru Hans Poppe wa Simba SC akamatwe.


Leo April 30, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kwamba mwenyekiti wa usajili wa Simba SC, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani kuunganishwa katika kesi inayomkabili Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Kaburu.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.

Swai amedai amewatafuta washtakiwa hao toka mwezi wa tatu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washtakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Washtakiwa hao wameongezwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ .

Post a Comment

Previous Post Next Post