Kocha Msaidizi wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa jana Simba walikuwa kwenye kiwango bora sababu walikuwa wanajitambua.
Akizungumzia mchezo huo, Julio ameeleza kuwa Simba hawakustahili kupata ushindi huo kiduchu bali wangeweza kufunga kufunga hata bao tano.
Kocha huyo aliyewahi kuifundisha Simba kama Msaidizi, amesema kuwa Yanga walitakiwa kufungwa zaidi ya bao moja kutokana na nafasi nyingi Simba walizozitengeneza lakini hawakuweza kuzitumia vizuri.
Aidha Julio amesema Yanga pia waliweza kutengeneza baadhi ya nafasi ambazo kama wangezitumia vizuri wangeweza kujipatia mabao kadhaa lakini bahati mbaya hawakufanikiwa.
Mbali na nafasi, Julio ameeleza pia kuwa Simba walikuwa bora Uwanjani kuliko Yanga kutokana na upana wa kikosi cha wachezaji walichonacho hivi sasa tofauti na misimu miwili mitatu nyuma.
Simba walibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Erasto Nyoni katika dakika ya 37 ya kipindi cha kwanza.
Tags:
Michezo