Prof Jay Apewa Ahadi Hii na Waziri.

Prof Jay Apewa Ahadi Hii na Waziri
Wizara ya Nishati kupitia Naibu Waziri wake Subira Mgalu imemuahidi Mbunge wa Mikumi Joseph Haule  (Prof Jay) kwamba itapeleka umeme katika jimbo lake la Mikumi kupitia Mradi wa Umeme wa Vijijini, (Rea) awamu ya tatu, katika mzunguko wa kwanza.


Ahadi ya Wizara hiyo imekuja leo baada ya Mbunge huyo ni lini serikali itapeleka umeme katika jimbo lake la Mikumi ambalo limebarikiwa kuwa na mbuga za wanyama zilizosheheni vivutio mbalimbali.

Mh. Mgalu amesema kuwa jimbo hilo lina jumla ya vijiji 57 na kati ya hivyo vijiji 16 tayari vina umeme wakati vijiji vinane umeme utapelekwa mapema zaidi.

Naibu Waziri amesema kazi ya kupeleka umeme kwa vijiji vinane kwa kuanzia, itahusisha ujenzi wa kilomita 26 za njia ya msongo wa kilovoti 33 na kilomita 32 njia ya umeme wa msongo wa kilovoti 0.4 

Post a Comment

Previous Post Next Post