Rapa Stamina na mchumba wake wafunga ndoa, Roma na mkewe wanogesha harusi (+picha)

Hatimaye rapa Stamina amefunga ndoa  na mchumba wake wa muda mrefu ajulikanaye kwa jina la Veronica jana Mei 05, 2018 mjini Morogoro katika kanisa la Mtakatifu Consolata lilipo maeneo ya SUA mjini humo.

Stamina na mkewe Veronica wakivishana pete.
Kwenye harusi hiyo, Wasimamizi walikuwa ni swahiba wake Roma Mkatoliki na Mkewe Nancy ni kwa mujibu wa maelezo ya Stamina.
Mwaka jana rapa Stamina alimvisha pete ya uchumba mchumba wake huyo, Bongo5 inawatakia kila la kheri katika maisha yenu mapya ya ndoa.
Tazama baadhi ya picha hapa chini za tukio hilo.
Picha by Clouds Digital

Post a Comment

Previous Post Next Post