Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na mwanamke yeyote maarufu nchini Tanzania na matukio yote ambayo yalikuwa yanatokea kipindi cha nyuma yalikuwa ni kiki tu.
Ommy Dimpoz amedai kuwa hajawahi kutoka kimapenzi na wanawake yeyote maarufu wa kibongo na hata stori za kutoka kimapenzi na Wema Sepetu haikuwa kweli.
“No, Sijawahi ku-date na msichana yeyote maarufu hapa Bongo, sijawahi.“ameeleza Ommy Dimpoz kwenye mahojiano yake na kituo cha Radio Times FM kwenye kipindi cha The Playlist.
Kwa upande mwingine, Ommy Dimpoz amefafanua kuhusu watu wanaomsakama mitandaoni kwa kuhoji kuhusu safari zake za nje ya nchi ambazo watu wengi wanaamini kuwa kuna mtu nyuma yake anayempa mkwanja.
Ommy amesema wabongo wengi hawatumii akili kwani wanashindwa kutofautisha jina la Ommy Dimpoz na Omary kwani safari zote anazofanya nje ya nchi huwa anaenda kikazi.
“Watu hawatumii akili..mtu anashindwa kujiuliza kitu kimoja mimi ni Ommy Dimpoz sio Nobody, kwahiyo katika jina langu nafahamiana na watu wengi na kuna mambo mengi tunafanya. Yusiishi kwa kufikiria yaani kama mtu ananifuatilia mimi utaumiza kicha.“amesema Ommy Dimpoz.
Tags:
Burudani