Mataifa ya Afrika Mashariki kupambana kufuzu CHAN 2020


Michuano ya soka mzunguko wa kwanza, kuwania fainali ya bara Afrika kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani mwaka 2020 nchini Cameroon, itachezwa mwishoni mwa wiki.

Mataifa 16 yatashiriki katika michuano hiyo na yatafuzu kutoka kanda zote za mchezo wa soka barani Afrika. Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, itatoa mataifa mawili yatakayofuzu katika michuano hiyo, na mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini katika mzunguko wa kwanza na wa pili.

Rwanda na Sudan tayari zimefuzu katika mzunguko wa pili na zinasubiri wapinzani wao mwezi Septemba. Leo Ijumaa, Djibouti watamenyana na Ethiopia, huku Burundi wakiwakaribisha Sudan Kusini na Somalia dhidi ya Uganda kesho Jumamosi.

Siku ya Jumapili, Tanzania itamenyana na Kenya jijini Dar es salaam kabla ya mechi ya marudiano siku ya mapema mwezi Agosti jijini Nairobi.

Fainali ya kwanza ya CHAN iliandaliwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast na DRC kuwa mabingwa wa kwanza. Morocco walikuwa wenyeji walikuwa wa mwisho kuandaa michuano hii mwaka 2018.

Post a Comment

Previous Post Next Post