Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Athumani Selemani Mbuttuka kuwa wa Msajili wa Hazina.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa. Mbuttuka utaanza Juni 6, 2018.
Aidha, kabla ya uteuzi huo, Mbuttuka alikuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Taifa (DAG) katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT).
Mbuttuka anachukua nafasi ya Dkt. Oswald Mashindano ambaye tayari amekwisha staaafu.
Tags:
Habari